News and Events

Tunajivunia kuwa nawe Mtoto wetu CHEKENI, Malengo yako yatatimia InshaAllah!

Licha ya changamoto ya kutokuwa na mikono, hilo halikuwa kikwazo kwa binti jasiri Chekeni katika kupambania ndoto na malengo yake maishani. Ujasiri, bidii, na imani yake vimekuwa somo kubwa kwa wengi kuhusu maana halisi ya kutokata tamaa.

Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) pamoja na wadau wengine, tunajivunia kuwa nawe katika safari hii ya mafanikio. Tunaahidi kuendelea kukuunga mkono na kukuombea kila la kheri katika safari yako ya kielimu na kimaisha.

Tunaomba Mwenyezi Mungu akujaalie afya njema, nguvu, na mafanikio makubwa katika kutimiza malengo yako.

Tunajivunia wewe, Mtoto wetu Chekeni — kielelezo cha matumaini na uthubutu