Maadhimisho ya Miaka 20 ya MUM
Watanzania wote mnakaribishwa katika Tukio kubwa la Maadhimisho ya Miaka 20 ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).
Tukio hili litafanyika tarehe 20 Juni, 2025 ambayo itakuwa siku ya kilele baada ya kutanguliwa na matukio mbalimbali yatakayoanza tarehe 11 Juni, 2025 kama shughuli za utangulizi kuelekea siku ya kilele cha Maadhimisho.
Miongoni mwa matukio yatakayofanyika ni pamoja na Mashindano ya Michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu na mingineyo ambapo timu kutoka Taasisi mbalimbali zitashindana kuanzia tarehe 11-17 Juni, 2025 katika viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro, watu wote wanaruhusiwa kuhudhuria kushuhudia michuano hii ya aina yake.
Tarehe 18 Juni, 2025 kitafanyika Kikao cha Wahitimu waliowahi kusoma Chuoni hapa pamoja na Kikao cha Taasisi za Kiislamu. Vikao vyote hivi vitafanyika Choni MUM.
Tarehe 19 Juni, 2025 kutakuwa na tukio la uzinduzi wa Jengo la ICT , Kongamano la Wanazuoni wa Kiislamu pamoja na tukio kubwa la Dua Maalum kwa ajili ya kuliombea Taifa letu, Raisi na Chuo chetu. Tukio hili la kipekee litahusisha viongozi mbalimbali wa Kitaifa na watu wote wanahimizwa kushiriki hafla hii itakayofanyika Chuoni MUM.
Tarehe 20 Juni, 2025 itakuwa ndio siku ya kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya MUM ambapo yatafanyika matukio kadhaa, tukio la mwanzo ni Utoaji tuzo kwa watu mbalimbali wakiwemo Waasisi wa Chuo chetu, Wahitimu na Viongozi wa Kitaifa, Uzinduzi wa Makala Maalum itakayoonesha safari ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro tangu kuanzishwa kwake na matarajio katika miaka ijayo, Tukio la uzinduzi wa Mfuko maalum wa maendeleo ya Chuo (MUM COMMUNITY FUND) na kuhitimishwa na Hotuba kutoka kwa Mgeni Rasmi.
KARIBUNI SANA.