Rais wa Al-Hikma Foundation Sheikh Abdulqadir na Masheikh kutoka nchini Kenya watembelea MUM
Rais wa Taasisi ya Al- Hikma Foundation Sharif Shekh Abdulqadir Mohammed Al-Haajar akiambatana na viongozi wengine wa Taasisi hiyo wametembelea Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kujionea shughuli mbalimbali za kitaaluma zinazoendeshwa Chuoni hapo.
Katika Ziara hiyo iliyofanyika Septemba 2, 2025, Shekh Abdulqadir amepokelewa na Mwenyeji wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Profesa Hamza Njozi pamoja na Viongozi wengine kutoka Idara na vitivo vilivyopo Chuoni hapo akiwemo Mkuu wa Kitivo cha Maarifa ya Uislamu Dkt. Bilal Juma Majuva.
Pamoja na mambo mengine Ugeni huo umetembelea na kujionea Miundombinu mbalimbali ya Chuo na kupata ufafanuzi wa namna inavyotumika kuhudumia wanafunzi wanaosoma Chuoni hapo.
Shekh Abdulqadir ameushukuru Uongozi wa Chuo kwa kukubali kuupokea Ugeni huo kutoka Taasisi ya Al-Hikma huku Prof. Njozi akiiomba Taasisi hiyo na nyingine kutembelea wakati wowote kujionea Maendeleo ya Chuo chao.