News and Events

MASOMO YA STASHAHADA(DIPLOMA) YA USIMAMIZI WA BANDARI NI FURSA YA KUFANYA KAZI NDANI NA NJE YA TANZANIA

MASOMO YA STASHAHADA(DIPLOMA) YA USIMAMIZI WA BANDARI NI FURSA YA KUFANYA KAZI NDANI NA NJE YA TANZANIA

Hivi karibuni Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha NETHERLANDS MARITIME UNIVERSITY COLLEGE (NMUC) vimesani makubaliano ya kuanzisha rasmi masomo ya usimamizi wa Bandari ambayo yatafundishwa kwa njia ya Mtandao.

Kuanzishwa kwa masomo haya ni fursa kwa wanafunzi wa Kitanzania na wasio Watanzania kujifunza biashara hii ya usafirishaji kwa njia ya Maji kupata weledi katika fani yenye wigo mpana wa kufanya kazi ndani na nje ya Nchi.

NMUC kilichopo nchi Malaysia ni Chuo maarufu kwa ufundishaji wa fani hii ya usimamizi wa bandari ambapo kupitia makubaliano haya sasa Chuo hiki kitatoa wataalamu wake wabobezi kufundisha wanafunzi watakaojiunga na masomo haya kwa kuanzia ngazi ya Stashahada (Diploma)