BALOZI WA CHINA ALIVYOTEMBELEA MUM NA MIKAKATI KABAMBE
Ilikuwa ziara ya Matumaini kwa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro pale ilipompokea Balozi wa China hapa nchini Chen Ming Jian Novemba 27.
Pamoja na mambo mengine, Safari ya Balozi Cheng ilijikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya Taifa la China na Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro ikiwa ni moja ya vituo muhimu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya Lugha na Utamaduni wa Kichina.
Balozi Cheng amevutiwa na namna wanafunzi wa MUM wanavyoitumia vyema fursa ya kujifunza Lugha ya Kichina na kupata fursa ya masomo Nchini China ambapo takribani wanafunzi 19 kutoka MUM wapo huko Uchina kupitia ufadhili wa masomo uliotokana na kufanya vizuri katika Lugha ya Kichina.
Mbali na hayo Balozi Cheng akiwa na wenyeji wake Prof. Mussa Assad (Makamu Mkuu wa Chuo) na Prof. Hamza Njozi (Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma) ameahidi kuimarisha Miundombinu ya kujifunzia Chuoni hapo ikiwemo kumbi za kufanyia Mihadhara ya Kitaaluma pamoja na kituo cha kufundisha Lugha ya Kichina kilichopo Chuoni hapo.