MUM News and Events

Raisi wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Wislamu cha Morogoro (wa pili kushoto) akiwa na wajumbe wake baada ya kuapishwa.

Posted on: 22 July, 2020

Rais mteule wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha waislamu cha morogoro  Hamis Juma Hamis ameapishwa July 21 baada ya uchaguzi uliofanyika july 19 mwaka huu.

Hamis ameshinda kwa kura 703, dhidi ya wapinzani wake wawili Shamsi Athumani Kiseka aliyepata kura 609 na Hassan kondoe aliyepata kura 158.

Baada ya kula kiapo Rais huyo alipata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi pamoja na wajumbe wa tume ya uchaguzi ambapo amewaomba kumpa ushirikiano wa hali na mali ili aweze kuongoza kwa weledi kwa kuzingatia kanuni , sheria na miongozo ya chuo hicho.

Naye aliyekuwa mpinzani wake Hassan Kondoe amemtaka rais huyo kuungana na washindani wake kwa kuweka kando tofauti za kisiasa ili kuleta chachu ya maendeleo kwa maslahi ya wanafunzi.

Baadhi ya wapiga kura ambao ni wanafunzi wameelezea kufurahi kwa kupata kiongozi ambae ametokana na chaguo lao na wameahidi kumpa ushirikiano wa hali ya juu katika kulinda miongozo, kanuni na sheria za chuo.