MUM News and Events

Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUMSO) wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Benki ya NMB nje ya jengo la tehama

Posted on: 19 August, 2020

NMB kujenga ATM ndani ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro


Serikali ya jumuiya ya wanafunzi wa chuo kikuu cha waislamu Morogoro (MUMSO) imeiomba Benki ya NMB kuwajengea kituo kidogo cha kufanyia miamala ya kibenki maarufu ATM ndani ya chuo hicho. Ombi hilo limetolewa Agosti 18 mwaka huu wakati wa kikao cha Baraza la mawaziri la MUMSO kilichokaliwa katika majengo ya ICT ndani ya chuo hicho.

Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi wa serikali akiwemo Rais MUMSO Hamisi Juma Hamisi, Makamu wa Rais Abdallah Mpyana, Waziri Mkuu Shabani Ruwaza na Mwenyekiti aliemaliza Muda wake Said Maduka. 

Aidha kikao hicho kimehudhuriwa na Meneja wa benki ya NMB tawi Mount Uluguru Mkoani Morogoro  Paul Nyoni na Meneja mauzo wa kanda Buhatwa Ladislaus. Viongozi hao wameiahidi MUMSO kushuhulikia maombi na mapendekezo yao. Hata hivyo Rais Hamisi na serikali yake wame ahadi kushirikiana kwa karibu na Bank hiyo.