MUM News and Events

MUM yatoa salamu za rambirambi kifo cha aliyekuwa raisi wa awamuya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa

Posted on: 25 July, 2020

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA ALIYEKUA RAIS WA AWAMU YA TATU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. BENJAMIN WILLIAM MKAPA.

Kwa niaba ya jumuiya  ya wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro,

Natumia fursa hii kutoa salamu za rambirambi kwa watanzania wote kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamini William Mkapa.

Lakini vilevile tunawatakia wanafamilia wote subra katika kipindi hiki cha msiba huu mzito.

Rais Mkapa mbali ya kuwa Rais wa Watanzania wote, sisi kama wanajumuiya ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro tutamkumbuka sana Mhe. Mkapa kwa nafasi yake ya kipekee kwa kuwepo Chuo chetu.

Rais Mkapa ndiye ambaye aliyatoa majengo ya kilichokuwa Chuo cha ufundi cha TANESCO Mkoani Morogoro kutumika kuanzisha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro mnamo mwaka 2004.

Pia yeye ndiye aliyekuja hapa Chuoni katika uzinduzi wa Chuo hiki mwaka 2005.

Aidha yeye ndiye alikuwa Mgeni rasmi wa kwanza katika Mahafali yetu ya kwanza ya kuwatunuku Shahada wanafunzi 165 wa awamu ya kwanza ya Chuo chetu.

Hivyo  Rais Mkapa atakumbukwa sana na atakuwepo daima katika kumbukumbu zetu za Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kwa mchango Mkubwa alioutoa kwa Chuo hiki.


Prof. Hamza M. Njozi

Kny Makamu Mkuu wa Chuo