• graduates.jpg
  • graduation__day.jpg
  • president.jpg

Nafasi za Masomo kwa Cheti & Diploma

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma), Chuo Kikuu cha Waislam cha Morogoro, anawatangazia wanafunzi wote waliomaliza kidato cha nne na cha sita; nafasi za masomo katika ngazi za Astashahada na Stashahada. Kozi zinazofundishwa ni:

NA

KOZI

ALAMA ZA CHINI ZINAZOHITAJIKA KWA AJILI YA KUJIUNGA

1

Astashahada na Stashahada ya Sayansi na Teknolojia ya Maabara (Certificate & Diploma in Science & Laboratory Technology)

Mwombaji wa Astashahada awe amefaulu masomo manne ya kidato cha nne (Yakiwemo masomo mawili kati ya “Physics, Chemistry, Biology”, na masomo ya dini hayazingatiwi) na Mwombaji wa Stashahada awe amefaulu Masomo mawili ya sayansi ya kidato cha sita kwa jumla ya alama 1.5

2

Astashahada na Stashahada ya Ununuzi na Ugavi (Certificate & Diploma in Procurement & Logistics Management)

Mwombaji wa Astashahada awe amefaulu masomo yoyote manne ya kidato cha nne (Masomo ya biashara ama Hesabu yanapendekezwa zaidi, na masomo ya dini hayazingatiwi) na Mwombaji wa Stashahada awe amefaulu Masomo mawili ya kidato cha sita kwa jumla ya alama 1.5

3

Astashahada na Stashahada ya Uendeshaji wa Benki Kisharia’h na Utunzaji wa Fedha (Certificate & Diploma in Islamic Banking & Finance)

Mwombaji wa Astashahada awe amefaulu masomo yoyote manne ya kidato cha nne (Masomo ya biashara ama Hesabu yanapendekezwa Zaidi, na somo la Maarifa ya Uislaamu linakubaliwa) na Mwombaji wa Stashahada awe amefaulu Masomo mawili ya kidato cha sita kwa jumla ya alama 1.5

4

Astashahada na Stashahada ya Uandishi wa Habari (Certificate & Diploma in Journalism)

Mwombaji wa Astashahada awe amefaulu masomo manne ya kidato cha nne (likiwemo somo la Kiingereza na masomo ya dini hayazingatiwi) na Mwombaji wa Stashahada awe amefaulu Masomo mawili ya kidato cha sita kwa jumla ya alama 1.5

5

Astashahada na Stashahada ya Sheria na Shariah (Certificate & Diploma in Law with Shariah)

Mwombaji wa Astashahada awe amefaulu masomo yoyote manne ya kidato cha nne (somo la Maarifa ya Uislaamu linakubaliwa) na Mwombaji wa Stashahada awe amefaulu Masomo mawili ya kidato cha sita kwa jumla ya alama 1.5

6

Astashahada na Stashahada ya Uhasibu (Certificate & Diploma in Accountancy)

Mwombaji wa Astashahada awe amefaulu masomo manne ya kidato cha nne (ikiwemo hesabu, masomo ya dini hayazingatiwi) Mwombaji wa Stashahada awe amefaulu Masomo mawili ya kidato cha sita kwa jumla ya alama 1.5

7

Astashahada na Stashahada ya Utawala wa Biashara (Certificate & Diploma in Business Administration)

Mwombaji wa Astashahada awe amefaulu masomo yoyote manne ya kidato cha nne (Masomo ya biashara ama Hesabu yanapendekezwa zaidi, na masomo ya dini hayazingatiwi) na Mwombaji wa Stashahada awe amefaulu Masomo mawili ya kidato cha sita kwa jumla ya alama 1.5

8

Stashahada ya Teknolojia ya Maabara ya Afya (Diploma in Medical Laboratory Technology)

Mwombaji awe amefaulu masomo ya “Physics, Chemistry, Biology, Mathematics & English” angalau kwa alama D

9

Stashahada ya Teknolojia ya Maabara ya Afya – Wanaojiendeleza (Diploma in Medical Laboratory Technology - Upgrading)

Mwombaji awe amefaulu masomo ya “Physics, Chemistry, Biology, Mathematics & English” angalau kwa alama D na awe amemaliza “Technician Certificate in Medical Sciences” (NTA LEVEL 5)

NAMNA YA KUOMBA CHUO.

Maombi yote yanafanyika katika tovuti ya chuo www.mum.ac.tz ama tembelea mfumo wa maombi application.mum.ac.tz

ADA YA MAOMBI

Gharama za maombi ni tshs. 25,000/= inayotakiwa kulipwa katika Bank ya NBC, namba ya akaunti ni 026103006147,na jina la akaunti ni MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO.

Tuma risiti ya bank (Bank Pay-in Slip) katika email This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. ama ipige picha na itume kwa whatsapp 0785330002 ama 0715202911 (kumbuka kuandika jina lako kamili)

Our Hotlines

For inquaries about MUM Please Call:

Admissions Office:                           

0715202911             

0785330002

Examination Office:                       

0714135201